Mfumo wa OAGMIS rasmi kwa Mwanasheria Mkuu

0
214

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua mfumo wa kieletroniki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAGMIS), utakaotumiaka kuboresha sekta ya sheria.

Rais amezindua mfumo huo mkoani Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa chama cha Mawakili wa Serikali.

Mfumo huo uliotengenezwa na vijana wa kitanzania moja ya kazi zake ni kuratibu kuingia na kutoka kwa taarifa za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo kwa sasa utaanza kutumika kwa kufanya sajili mbalimbali.

Kazi nyingine ni kuorodhesha mikataba yote inayoingiwa na Serikali pamoja na kurekebisha au kutoa maoni ya mikataba ambayo Serikali inaingia ili kupunguza muda na gharama kwa kuwa kila sekta itaweka mikataba yake kwenye mfumo huo kwa ajili ya mapitio na maoni ya wadau.

Mfumo wa OAGMIS pia utafuatilia ugawaji wa kazi za Mawakili ndani ya sekta hiyo kwa kuwezesha kufahamu nani anafanya nini na kwa muda gani, na
utabeba sheria zote za nchi ambapo wananchi wataweza kuzifikia na kuzirejea kwa wepesi.

Mfumo wa OAGMIS utafanya kazi sawa na ule mfumo wa Mahakama (JSDS2).