Miamba ya masumbwi hapa nchini Mfaume Mfaume na Idd Pialali watapanda ulingoni hii leo katika ukumbi wa AICC jijini Arusha katika pambano lililopewa jina la Usiku wa Mabingwa.
Miamba hiyo ya masumbwi nchini watachuana kuwania mkanda wa ubingwa wa uzito wa kati katika pambano la raundi 10.
Pambano hilo litasindikizwa na mapambano mengine likiwemo la mtu kazi Karim Mandonga dhidi ya Alibaba Tarimo.
Usiku wa Mabingwa ni mwendelezo wa mapambano ya ngumi ambayo yameurejesha mchezo huo kwenye ramani yake ambayo ilipotea mwanzoni mwa miaka ya 2000.