Membe aahidi kurasimisha biashara ya kangomba akishinda

0
446


Bernard Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo amesema kuwa akichaguliwa atahakikisha anajenga barabara hasa za mitaa ambazo kwa muda mrefu zimetelekezwa na kuwawezesha wakulima.

Aidha, amesema atahakikisha wakazi wa kusini wanapata bei ya juu katika zao la korosho ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaofanya biashara ya Kangomba hawabughudhiwi.

“Uchumi unaendeshwa na watu wa kati, hawa unaweza kuwaita middle men au brokers. Hata hao tunaowauzia korosho ni kangomba wa kimataifa, sasa kwanini kangomba wa Lindi asumbuliwe?” amesema Membe.

Ameongeza kuwa serikali yake itasimamia huduma za afya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inawalipia wananchi 1/3 ya bima ya afya na mtu akifariki, maiti haitochajiwa fedha kutolewa hospitalini.