Meli yenye mitambo ya mradi wa EACOP yawasili

0
186

Meli kubwa ya kwanza MV Innovation Way kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu iliyobeba mitambo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP)
kutoka Hoima, Uganda hadi mkoani Tanga
imewasili katika bandari ya Tanga.

Meli hiyo imebeba mitambo kwa ajili ya ujenzi wa gati kubwa la meli za mafuta litakalojengwa eneo la Chongoleani.