Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa ameitaka kamati ya kutafuta mdundo wa Taifa kukamilisha kazi hiyo mara moja, ili mdundo wa Tanzania uteke soko la Afrika na Dunia nzima.
Mchengerwa ameyasema hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya kamati hiyo na kuipongeza kwa hatua iliyofikia.
Amesema dhamira ya serikali ni kufanya uwekezaji mkubwa kwa wasanii wengi wa Tanzania ili wafike kwenye ngazi ya kimataifa kama mataifa mengine yanayofanya vizuri duniani.
Ameiagiza kamati hiyo ya kutafuta mdundo wa Taifa kuainisha wasanii 10 watakaosaidiwa na serikali, ambao wanatumia midundo hiyo kuandaa miziki itakayotambulisha mdundo huo wa Taifa.