Mchata, Mchechu na Kagulumjuli watia mguu uskauti mkuu

0
136

Mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dodoma, umepitisha majina matatu ya wagombea wa nafasi ya Skauti Mkuu ambayo yatawasilishwa kwa mlezi wa chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan Rais kwa ajili ya uteuzi.

Akitangaza matokeo hayo Rais wa Skauti ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ametaja majina ya wagombea nafasi hiyo ya Skauti Mkuu yaliyopendekezwa kuwa ni Rashid Mchata, Nehemia Mchechu na Aron Kagulumjuli.

Pia mkutano huo umechagua wajumbe wa bodi ambao ni Elizabeth Mkwasa, Kenedy Nsenga, Juma Dossa, Jacqueline Kawishe, George Miringai, na Tabia Mohamed.

Profesa Mkenda amesema mchakato wa kumpata Skauti Mkuu unaendelea, huvyo aliyepo sasa ataendelea na kazi na kuomba skauti kuendelea kushirikiana nae katika kipindi hiki ambacho atakuwa anahudumu.