Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) limepewa tuzo ya kituo cha televisheni cha umma kinachohamasisha na kubaini taarifa muhimu zinatohusu zao la korosho kwa msimu wa mwaka 2020/2021.
Tuzo hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda katika mkutano mkuu wa wadau wazao hilo nchini uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Tanzania Tawi la Mtwara.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi Korosho Tanzania, Francis Alfred amesema TBC imekuwa ikihabarisha umma kwa usahihi na kuelimisha kuhusu zao la korosho, jambo ambalo limesaidia wakulima wengi kupata elimu.
Mwandishi wa habari wa TBC mkoani humo, Martina Ngulumbi amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba Chacha na kusema amepokea tuzo hiyo kwa heshima kubwa na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi zaidi katika kuhabarisha umma juu ya zao hilo.