Mbunge ataka tozo ya shilingi 100 kwenye mafuta ili kujenga barabara DSM

0
173

Mbunge wa jimbo la Ukonga mkoani Dar es Salaam, Jerry Silaa ameishauri Serikali iweke tozo ya shilingi 100 kwenye kila lita ya mafuta yanayonunuliwa mkoani Dar es Salaam, ili kupata pesa za kujenga barabara za mkoa huo.

Silaa amesema hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Amesema mkoa wa Dar es Salaam unatumia zaidi ya lita milioni tatu kwa mwaka zinazouwezesha kupata shilingi Bilioni 130 kwa mwaka, zitakazotumika kujenga miundombinu ya barabara ndani ya mkoa huo.

Aidha Silaa amesema shilingi 100 itakayoongezwa katika kila lita moja ya mafuta italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa na kwamba wazo lake ataliwasilisha kwa waziri wa TAMISEMI na wizara ya Fedha.