Mbowe: Tutunze amani yetu

0
128

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amewataka Watanzania kutunza amani na utulivu uliopo hapa nchini, ili Tanzania iweze kusonga mbele katika nyanja mbalimbali.

Akitoa salamu za CHADEMA katika Baraza la Eid El Fitri Kitaifa lililofanyika mkoani Dar es Salaam, Mbowe amesema, Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umekuwa na mafundisho mengi ikiwa ni pamoja na kupendana na kuheshimiana na hiyo ndio silaha ya amani ya Tanzania.

Amesema kila mmoja ana jukumu la kulinda amani ya Taifa na hivyo kuwataka Watanzania wa imani zote kuendelea kuitunza amani na utulivu uliopo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuyaishi yale anayoyasimamia katika kuinganisha nchi.

Profesa Lipumba amemuomba Rais Samia kuwa na ujasiri zaidi katika kuongoza nchi na kuendeleza mshikamano anaoujenga kwa Watanzania.