Mbowe na Matiko waachiwa kwa dhamana

0
499

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam imewaachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini mkoani Mara, – Esther Matiko.

Mbowe na Matiko wameachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana katika mahakama hiyo.

Hukumu hiyo ya Mbowe na Matiko katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam imesomwa na Jaji Sam Rumanyika.