Mbowe aendelea kupatiwa matibabu baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa

0
485

Mwenyekiti Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya DCMC Ntyuka iliyopo mkoani Dodoma baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Habari kutoka jijini Dodoma zinaeleza kuwa Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amepata majeraha kadhaa ikiwa ni pamoja kuvunjika mguu.

Baadhi ya viongozi wamefika hospitalini hapo ili kumjulia hali Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.