Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali imepanga kuviwezesha viwanda vya hapa nchini vinavyozalisha mbolea kwa kununua mbolea yote itakayotolewa kwa ruzuku kwa Wakulima msimu huu.
Waziri Bashe amesema hatua hiyo itaiwezesha Serikali kudhibiti mbolea inayosambazwa kwa wakulima nchini lakini pia ina lengo la kuweka udhibiti wa karibu wa mbolea yote inayotolewa kwa ruzuku.
Akifunga maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani katika viwanja vya Nanenane mkoani Tabora, Waziri Bashe amesema hatua hiyo itaviwezesha pia viwanda vya ndani vinavyozalisha mbolea kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa hiyo.
Ameongeza kuwa ucheleweshaji uliojitokeza msimu ulipita wa kufikisha mbolea kwa wakulima kwa wakati, hautakuwepo msimu huu kutokana na mbolea yote kununuliwa hapa nchini.