Mbegu za mkonge kupatikana kwa urahisi

0
133

Wakazi wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga, wamesema uwepo wa ajira katika kituo cha utafiti wa kilimo cha Tari Mlingano umesababishwa na uwekezaji uliofanywa na serikali kupitia waziri mkuu Kassim Majaliwa juu ya ufufuaji wa zao la mkonge.

Wakulima hao wametoa kauli hizo mara baada ya kutembelewa na TBC shambani hapo.

Wamesema kwa sasa hali zao za kimaisha zimebadilika kutokana na uwepo wa ajira zinazodumu kwa msimu mzima wa mwaka.

“Kwa kweli tunaishukuru saana serikali hasa waziri mkuu kuja hapa kwetu na kufufua upya zao la Mkonge hivi sasa hatuna shida tena ya ajira” Wamesema wakulima

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kituo cha utafiti wa kilimo cha Tari Mlingano Dkt. Catherine Senkoro, amesema wamefanikiwa kupanda zaidi ya hekta sitini kwa mwaka, na jumla ya miche waliopanda ni milioni nne na laki nane tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikua wakipanda miche laki tano pekee.

Aidha Dkt. Senkoro ameongeza kwa kusema kuwa mbegu za mkonge zinazopatikana kituoni hapo ndizo mbegu bora dununiani.

Bertha Mwambela- Tanga