Mbatia asisitiza amani kuelekea uchaguzi mkuu

0
331

Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia ametoa wito kwa wadau wote watakaoshiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu kuhakikisha wanahamasisha suala la amani katika kipindi chote cha uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama hicho unaofanyika jijini Dar es salaam, Mbatia amesema kuwa NCCR-Mageuzi itaendelea kuhamasisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi.

Mbali ya kujadili masuala mbalimbali na kutoa muelekeo wake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, mkutano huo pia umepokea wanachama wapya.