Mbaroni kwa kukutwa na dawa za kulevya

0
220

Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Justine Masejo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdi Hamis (27) mfanyabiashara na mkazi wa Ngarenaro na Ally Said (25) dereva na mkazi wa Olasiti.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na polisi waliokua doria wakisafirisha dawa hizo za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 70.77.

Kwa mujibu wa Kamanda Masejo, uchunguzi wa awali umebaini kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihushisha na biashara hiyo kwa muda mrefu.

Jeshi la polisi mkoani Arusha linaendelea na upelelezi na pindi utakapokamilika hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.