Mbarawa : Usafiri wa anga ni salama

0
332

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema hali ya usafiri wa anga nchini ni salama, na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na usafiri huo.

Amesema tukio la ajali ya ndege mali ya Shirika la Ndege la Precision Air lilitokea hapo jana na kusababisha vifo vya watu 19 ni bahati mbaya.

Amesema serikali itahakikisha tukio kama hilo halitokei tena na usafiri wa anga unaendelea kuwa salama.

Profesa Mbarawa alikuwa akizungumza wakati wa shughuli ya kuaga miili ya watu 19 waliofariki dunia katika ajali ya ndege mkoani Kagera, shughuli iliyofanyika katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo na uchunguzi utakapokamilika taarifa itatolewa.

Amesema wakati uchunguzi ukiendelea, ni vema watanzania wakaendelea kuwa watulivu, wakisubiri matokeo ya uchunguzi huo.

Waziri huyo wa Ujenzi na Uchukuzi amesema kwa sasa uwanja wa ndege wa Bukoba ni salama na ndege ndogo zinaweza kutua.

Amesema leo jioni ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) zitaanza kutua katika uwanja huo