Mbarawa: TBA imefanya mapinduzi makubwa

0
144

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ametoa pongezi kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kukamilisha ujenzi wa Majengo mawili ya makazi katika maeneo ya Magomeni na Msasani Peninsula Masaki yaliyojengwa na TBA kama Mkandarasi na Mshauri Elekezi.

Ameongeza kwa kusema kuwa TBA imefanya mapinduzi makubwa ya kiutendaji, kuongeza ubunifu na kujenga majengo mazuri yenye miundombinu ya kisasa kwa lengo la kuongeza mapato zaidi na kuwataka kuongeza miradi mingine mingi kama iliyojengwa Masaki na Magomeni Kota.

Prof. Mbarawa ametoa pongezi hizo wakati wa Hafla ya Ufunguzi wa Nyumba za Makazi katika Maeneo ya Magomeni Kota na Msasani Peninsula, Masaki zilizojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) jijini Dar es Salaam.

Majengo yote mawili yamegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 10.32 hadi kukamilika kwake na kuwataka wapangaji watakaokuja kuishi katika nyumba hizo kuhakikisha wanazitunza pamoja na kulipa kodi ya pango kwa wakati.