MBAGALA, MBEZI MWISHO, BAGAMOYO
BIASHARA SAA 24

0
142

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema ni wakati sasa wa kufikiria namna ya kuwezesha biashara kufanyika saa 24 katika maeneo muhimu mkoani humo ambayo ameyapa jina la ‘lango’.

Chalamila alikuwa akizungumza katika mahojiano maalum kwenye TBC Aridhio.

“Ni vizuri tuka connect abiria sasa na masoko yetu ya Kariakoo ili kule Kariakoo watu watakapofika sasa biashara nako ziwe saa 24….., lakini zaidi tumesema ili lango la kutoka mikoa ya Lindi – Mtwara pale Mbagala napo pale tuwaze biashara zetu kuwa saa 24…..lakini hili lango pia la kutoka Morogoro kuingia Ubungo….kule Mbezi Mwisho kule nako ni vizuri tukawaza biashara za saa 24.”

“Lakini lango la kutoka Bagamoyo napo tuangalie some where [mahali] nako biashara ziwe za saa 24.”