Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein ameitaka kamati ya mawaziri wenye dhamana ya usimamizi wa masuala ya maafa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuandaa mikakati imara ya kuzuia maafa katika nchi wanachama.
Dkt Shein ametoa kauli hiyo mjini Unguja wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kamati hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama amesema kuwa lengo la kamati hiyo ni kutunga sera na kupanga mikakati imara ya kuzuia maafa katika nchi za SADC.