Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewatembelea wafanyabiashara wadogo wa soko la Sabasaba ambao vibanda vyao viliungua kutokana na ajali ya moto na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa na upotevu wa mali za wafanyabiashara zaidi ya 29.
Mavunde ametumia fursa hiyo kuwapa pole wafanyabiashara hao kwa janga hilo ya moto na upotevu mkubwa wa bidhaa zao na kuwachangia bati 52 zenye thamani ya Tsh 1,200,000 ili kurejesha vibanda vyao katika hali ya Kawaida.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amewataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanapata taarifa za tukio la moto kutoka mamlaka husika kwa ajili ya uthibitisho kwenda Taasisi za fedha ambazo wafanyabiashara wengi wamekopa na kutumia nafasi hiyo hiyo kuwaagiza TANESCO kutoa elimu ya masuala ya umeme na kuwaunganishia umeme wafanyabiashara hao kwa utaratibu.

