Mavunde aingilia kati mgogoro wa wafanyakazi na uongozi Impala Hoteli

0
166

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde ameingilia kati mgogoro wa Kazi kati ya wafanyakazi wa Hoteli za Impala na Naura dhidi ya mwajiri wao kufuatia malalamiko ambayo yaliwasilishwa ofisi ya Kazi kuhusu ucheleweshwaji wa malipo na stahiki mbalimbali za wafanyakazi hao.

Naibu Waziri Mavunde ambaye aliongozana na Kamishna wa Kazi Kanali Francis Mbindi, baada ya kusikiliza pande zote mbili ameagiza kuwa Ifikapo Machi 31, Wafanyakazi wote wawe wamelipwa mishahara yao yote.

Naibu waziri Mavunde amemuagiza Kamishna wa Kazi kusimamia utekelezaji wa Sheria za kazi katika Hoteli hizo hasa malipo ya ziada na likizo.

Aidha ameitaka NSSF kumfikisha Mwajiri huyo mahakamani mara moja kwa kushindwa kuwasilisha makato ya michango ya Wafanyakazi kwenye mfuko wa Hifadhi ya Jamii ilijali wafanyakazi hao kukatwa katika mishahara yao.