Mauzo ya bidhaa za Tanzania nje yapanda

0
151

Wizara ya Uwekezaji , Viwanda na Biashara imesema mauzo ya bidhaa kutoka Tanzania yameongezeka na kufikia kiwango cha dola za kimarekani bilioni 10.2

Akizungumza katika Hafla ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Godius Kahyarara amesema ziara anazoendelea kufanya nje ya nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, zimeendelea kuzaa matunda na sasa Tanzania inauza zaidi biadhaa zake nje ya nchi kuliko kununua kwa ukanda wa Afrika Mashariki