Maulid yafana Mwanza, neno amani latawala

0
183

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa rai kwa Watanzania wote kudumisha Amani, Umoja na Mshikamano ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa Rai hiyo jijini Mwanza wakati wa Baraza la Maulid  Kitaifa lililofanyika kwenye ukumbi wa BOT.
.
Waziri Mkuu ambaye ndiye alikua mgeni rasmi katika Baraza hilo, amewataka Viongozi wote wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu nchini kufuata mafundisho ya Mtume Muhammad SAW ambaye alikua akisisitiza suala la Amani, Umoja na Mshikamano.

Pia ametumia Baraza hilo la Maulid, kuwaomba Viongozi wa Dini ya Kiislamu nchini
kuangalia namna ya kuondoa migogoro katika baadhi ya Misikiti na Taasisi mbalimbali za Dini hiyo, migogoro ambayo imekua haileti picha nzuri.