Maudhui kuonekana katika akaunti zilizothibitishwa tu

0
183

Mtandao wa Twitter unatarajiwa kuja na udhibiti wa upatikanaji na muonekano wa maudhui kwa watumiaji wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mtandao wa kijamii wa Twitter Elon Musk ameeleza kuwa ndani ya wiki mbili zijazo watumiaji wa mtandao huo wataweza kuona maudhui kutoka kwenye akaunti zilizothibitishwa tu “verified” kupitia kipengele maalum cha kwa ajili yako ‘For you ’.

Kwa mujibu wa Musk, akaunti za Twitter zitazothibitishwa hivi karibuni zitakuwa tu zile ambazo zinalipa ada ya mwezi, akaunti za kampuni au zile zinazomilikiwa na taasisi za Serikali.

Kupitia ujumbe wa Twitter uliotumwa hivi karibuni, Musk amesema kuwa chini ya sera mpya ya kampuni yake, ni akaunti zilizothibitishwa pekee ndizo zitafanikiwa kuwa na kipengele cha kwa ajili yako ‘For you’.

Musk amesema njia hiyo ndio njia pekee ya kudhibiti makundi yanayotumia majukwaa ya teknolojia bandia yani ‘AI’.