Mauaji ya Dkt. Mvungi, washitakiwa watano wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

0
688

Watu watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya aliyekuwa mwanasheria maarufu nchini na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Sengondo Mvungi.

Hukumu hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam ambapo pia mahakama imemwachia huru mshitakiwa mmoja.

Marehemu Dkt. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Novemba 3, 2013 na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake jambo lililosababisha kifo chake akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.