Mauaji Kigoma, vifo vyaongezeka

0
177

Mtoto James January (4) aliyejeruhiwa katika tukio la mauaji ya watu sita wa familia moja katika kijiji cha Kiganza mkoani Kigoma amefariki dunia usiku wa kuamkia hii leo.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kigoma, Maweni Dkt, Stanley Binagi amethibitisha kifo cha mtoto huyo kilichotokea katika hospital ya mkoa wa Morogoro akiwa njiani kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Dkt. Binagi amesema mtoto huyo ambaye mwanzo alilazwa hospitalini hapo katika chumba cha wagonjwa Mahututi, alikuwa amejeruhiwa mgongoni na kwenye fuvu la kichwa na hivyo kufanya sehemu ya mwili wake kukosa mawasiliano.

Kifo cha mtoto huyo kinafanya idadi ya watu waliokufa katika tukio hilo la mauaji mkoani Kigoma kufikia saba.