Matokeo STD VII hadharani

0
54

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu, ambapo watahiniwa zaidi ya milioni 1.07 kati ya zaidi ya milioni 1.3 wamefaulu kwa kupata madaraja A na B na C.

Kati ya hao wasichana ni 558,825 ambao ni sawa na asilimia 78.91 na wavulana ni 514,577 sawa na asilimia 80.41.

Akitangaza matokeo hayo mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Almasi amesema katika matokeo ya mwaka 2021 watahiniwa walikuwa 907,802 sawa na asilimia 81.97.

Amesema kitakwimu kuna kupungua kwa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka 2021.

Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulifanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu.