Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kati imekamata aina saba za dawa za Serikali zenye nembo ya MSD Got zikiuzwa katika duka maarufu la dawa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Akitoa taarifa hiyo leo Alhamisi Machi 4, 2021 meneja mawasiliano kwa umma wa TMDA, Gaudensia Simwaza amesema dawa hizo zilikamatwa Machi 2, 2021 baada ya ukaguzi.
Amesema TMDA Kanda ya Kati ilikagua maeneo yenye maduka ya dawa na vifaa tiba kijiji cha Mpendoo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.
“Ukaguzi huo ulifanikisha kukamata dawa za Serikali aina saba zenye thamani ya Sh265,000 katika duka la dawa muhimu liitwalo Rogechu.
Mtuhumiwa amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Chemba ambapo anashikiliwa na Jeshi la Polisi. Taratibu nyingine za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zinaendelea,” amesema Simwanza.
