Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutathminiwa

0
537

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amewaagiza Wajumbe wa Bodi mpya ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kufanya tathmini ya Mashirika yaliyopo nchini ili kutambua shughuli zinazofanywa na mashirika hayo.

Dkt Ndugulile ametoa wito huo jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha  Bodi ya Nne ya uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambapo amesema kuwa baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakifanya kazi bila kuzingatia vipaumbele vya nchi.