Mashina kutumika kulea watoto kimaadili

0
143

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ameagiza ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwalea na kuwajenga watoto katika misingi ya kimaadili ya Kitanzania.

Chongolo ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wanachama wa CCM shina namba tano wilayani Ulanga, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro yenye lengo la kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo.

Awali Katibu wa shina hilo Raphael Boma alisema kwa sasa kumeibuka matukio mengi ya wizi na udokozi yanayofanywa na makundi ya vijana ndani ya wilaya hiyo, jambo linaloonesha kuwa hawajalelewa katika maadili.