Mariam Mwinyi akabidhi vifaa vya watoto Njiti

0
196

Mke wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi amekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuwatunzia watoto Njiti kwa hospitali ya wilayani ya Makunduchi.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Naibu Spika wa Baraza la wawakilishi Mgeni Hassan Juma kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi.

Vifaa hivyo kwa ajili ya kuwatunzia watoto Njiti vimetolewa na wafadhili mbalimbali wakiongozwa na wakfu wa Doris Mollel.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vitanda maalum vya kuwatunzia watoto Njiti na mashine za hewa ya oksijeni.