Mariam Mmbaga ateuliwa Katibu Tawala Simiyu

0
505

Rais John Magufuli amemteua Mariam Mmbaga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu.

Mmbaga anachukua nafasi ya Jumanne Sagini.

Kabla ya uteuzi huo, Bi. Mmbaga alikuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mteule huyo ataapishwa Jumatatu Julai 6, 2020 saa 4:00 asubuhi Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma.