Marekani: Polisi kuwajibishwa kwa makosa wanayotenda kazini

0
414

Meya ya Jiji la New York nchini Marekani, Andrew Cuomo amesaini muswada kuwa sheria ya kuwawajibisha polisi pale wanapofanya makosa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ikiwemo matumizi ya ubabe na nguvu za kupitiliza.

Sheria hiyo inatoa mamlaka ya kuwezesha kutolewa taarifa ya kumbukumbu za rekodi za matukio ya kinidhamu ya askari polisi pale inapobidi suala ambalo hapo awali rekodi hizo zilikuwa siri.

Kwa mujibu wa sheria hiyo malalamiko dhidi ya maafisa wa polisi waonevu, taarifa zao kuhusu rekodi za matukio ya kinidhamu yataweza kutolewa hadharani kutumika mahakamani dhidi ya wahusika.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni hatua kubwa ya mafanikio kufuatia maandamano ya kupinga mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Flyod aliyeuawa akiwa mikononi mwa polisi.

Mswada wa kutaka marekebisho katika sheria hiyo ulipitishwa wiki hii na Bunge linaloongozwa na wajumbe wengi kutoka chama cha Democratic.