Marekani : Kongole Tanzania mapambano UVIKO – 19

0
226

Balozi wa Marekani nchini Donald Wright amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua anazochukua za kudhibiti ugonjwa wa UVIKO – 19 tangu alipoingia madarakani.

Akizungumza katika mahojiano maalum na TBC mkoani Dar es Salaam, Balozi Wright ametaja moja ya hatua hizo kuwa ni kuhamasisha chanjo dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kuwa Marekani itaendelea kutoa ushirikiano na msaada wa chanjo ya ugonjwa huo.

Balozi Wright amesema milango ya Marekani ipo wazi kwa Watanzania wanaotaka kuingia nchini humo ambao wamezingatia vigezo vya safari ikiwa ni pamoja na kupata chanjo dhidi ya UVIKO -19.

Pia amepoipongeza Tanzania kwa kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru na kusema kuwa Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja zote.

Kwa upande wa biashara, Balozi Wright amesema Marekani inawakaribisha Watanzania kufanya biashara nchini humo na kusema angependa kuona bidhaa za Tanzania nchini Marekani kwani kuna fursa nyingi za kibiashara.