Mapokezi The Royal Tour Zanzibar ni gumzo

0
216

Kuelekea uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour huko Zanzibar, filamu hiyo yenye kuakisi maliasili na urithi wa Tanzania tayari imekua gumzo kila kona ya visiwa hivyo vya marashi ya karafuu na uchumi wa buluu.

Wachezaji wa vikosi vya KMKM na wababe wa ligi ya soka ya Zanzibar hawajabaki nyuma, nao wameungana na Watanzania wengine kuipokea filamu hiyo ya The Royal Tour na kuainisha namna itakavyochangia kukuza utalii wa Zanzibar pamoja na fursa za uwekezaji ambapo sekta zote zitanufaika ikiwemo ile ya michezo.

Wachezaji hao ambao wameonekana wakitazama vipande vya video vya filamu hiyo kwenye simu zao wamesema watahudhuria uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour ambapo kwa Zanzibar utafanyika hapo kesho Mei 07 katika hoteli ya Golden Tulip na kuwaomba Wananchi wengine Visiwani humo wajitokeze kushuhudia tukio hilo kubwa.