Mapenzi yanasababisha tatizo la afya ya akili

0
350

Daktari Praxeda Swai kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema kuwa hakuna kitu ambacho kinasababisha moja kwa moja
tatizo la afya ya akili, lakini vipo vitu mbalimbali vya kibaiolojia na kijamii ambavyo vinaweza kuchochea mtu kupata tatizo hilo.

Ametaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni uhusiano wa kimapenzi, kufukuzwa kazi, changamoto za kimaisha ikiwemo kunyanyapaliwa nyumbani, shuleni au maeneo ya kazi.

Aidha, ametaja vichocheo vingine kuwa ni ulevi wa pombe, matatizo ya kiafya ya kurithi na magonjwa sugu kama vile UKIMWI.

Dkt. Swai amesema hayo mkoani Dar es Salaam alipokuwa akichangia mada katika Mdahalo wa Kitaifa wa Afya ya Akili ulioandaliwa na wizara ya Afya.