Mapato ya Serikali yatokanayo na Gawio yaongezeka

0
251

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema kuwa , mapato yatokanayo na gawio na michango ya Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma kwa Serikali yamekua yakiongezeka mwaka hadi mwaka.

Dkt Mpango amefafanua kuwa mapato hayo yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 161.04 katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.05 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Waziri huyo wa Fedha na Mipango ameyasema hayo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, ambapo Rais John Magufuli anapokea Gawio, Michango na ziada ya Serikali kutoka Mashirika, Kampuni na Taasisi mbalimbali zinazomilikiwa na Serikali.

Amesema kuwa, kuongezeka kwa mapato hayo kunatokana na usimamizi na maelekezo mazuri kwa Viongozi wa Taasisi hizo, maelekezo ambayo yamekua yakitolewa na Rais Magufuli.