Mapato katika sekta ya madini yaongezeka

0
565

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali  Dkt Hassan Abbasi amesema kuwa,  maono na mtazamo yakinifu wa Rais John Magufuli katika usimamizi na ufuatiliaji wa sekta ya madini, umewezesha ongezeko maradufu la makusanyo ya mapato ya sekta hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Dkt Abbasi  amesema kuwa makusanyo hayo yameongezeka kutoka Shilingi  Bilioni 210 katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 hadi kufikia Shilingi Bilioni 302 kwa mwaka wa fedha wa  2018/2019 na kuifanya Tanzania kuzidi kujijenga kiuchumi.

Dkt Abbasi ameongeza kuwa serikali inafanya kazi kwa umakini na itahakikisha rasilimali za nchi zinaendelea kulindwa ili ziweze kuleta manufaa kwa Watanzania wote.

Amesema kuwa mara baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani mwaka  2015, ilifanya mageuzi mbalimbali katika usimamizi na ufuatiliaji wa rasilimali za madini, baada ya kuona kuwa katika kipindi cha nyuma ilikuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha fedha na kuamua kuchukua hatua stahiki ikiwemo kufanya mabadiliko katika sheria ya madini ya mwaka 2010.

“Tulipofanya marekebisho katika sheria yetu ya madini mwaka 2017, matokeo tumeanza kuyaona,  kwani tumedhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato yetu na kuanza kusimamia kwa umakini mkubwa utoroshaji mkubwa wa madini ambapo ilisababisha serikali kupoteza kiasi kikubwa cha mapato” amesema Dkt Abbasi.

Akitolea mfano Dkt Abbasi amesema kuwa kufuatia agizo la Rais John Magufuli la kuanzishwa kwa masoko ya madini ambayo ni utekelezaji wa sheria ya madini ya mwaka 2017, hadi sasa kuna jumla ya masoko 24 ambayo yamekuwa yakidhibiti ubora, thamani na takwimu za madini nchini, ambapo soko la kwanza lilianzishwa mkoani Geita, mwezi Machi mwaka huu.

Aidha, Dkt Abbasi amesema kuwa takwimu za jumla za uzalishaji wa dhahabu katika kipindi cha miezi miwili  mkoani Geita kuanzia mwezi Machi hadi Mei mwaka huu zinaonyesha kuwa uzalishaj umeongezeka na kufikia kilo 312.65za dhahabu ukilinganisha na uzalishaji wa dhahabu  kilo 259.12 zilizokuwa zikizalishwa kabla ya masoko hayo. Kwa mujibu wa Dkt Abbasi, eneo lingine la mageuzi yaliyofanywa na serikali katika sekta ya madini ni pamoja na maamuzi iliyochukua ya kujenga ukuta kuzunguka eneo la wachimbaji wa Madini ya Tanzanite mkoani Manyara ambapo serikali iliweka mifumo ya masoko na ukaguzi, na hivyo kuchangia ongezeko la mapato ya wachimbaji wadogo na serikali kwa ujum