Mapacha waliozama ziwani kuzikwa leo

0
153

Mapacha Kenny na Lenny Makomonde (24),
waliokufa maji ndani ya Ziwa Victoria, wanazikwa leo nyumbani kwao Bweri Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Kenny na Lenny ambao kabla ya kukutwa na umauti walikuwa Wanafunzi wa Chuo Cha Mipango Kampasi ya Mwanza, walikufa maji Mei 28, 2023 katika ufukwe wa Mihama wilayani Ilemela mkoani Mwanza walipokwenda kuogelea.

Miili ya mapacha hao iliopolewa kutoka ndani ya Ziwa Victoria na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakishirikiana na Wananchi Mei 29, 2023.