Serikali imeamua kusitisha kutumia mabadiliko ya mitaala mipya ya masomo katika shule za msingi na sekondari ili kuendelea kupokea maoni ya wadau wa elimu kuhusu mqboresho ya mitaala kwa ngazi ya awali msingi na sekondari.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Omary Kipanga jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa kupokea maoni ya wadau wa elimu kuhusu uboreshwaji wa mitaala ya ngazi ya elimu ya awali, msingi na sekondari.
Mkutano huo wa siku moja umewakutanisha Wadau mbalimbali wa elimu ili kutoa maoni ya kuboresha mitaala ya masomo itakayoendana na sayansi na teknolojia