Mamlaka mbalimbali zaagizwa kushughulikia changamoto za Wawekezaji

0
279

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji,- Angela Kairuki ameziagiza Mamlaka zote nchini zinazohusika na kuwahudumia Wawekezaji, kuhakikisha zinasikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wawekezaji hao.

Waziri Kairuki ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Viwanda na Biashara mkoani Pwani, maonesho yanayofanyika pamoja na Kongamano la Uwekezaji la mkoa huo.