Mamia wamzika Mzee Jengua

0
186

Mazishi ya msanii mkongwe wa filamu nchini Mohammed Fungafunga maarufu kama Mzee Jengua, yamefanyika hii leo kwenye makaburi ya Mburahati jijini Dar es salaam.

Mamia ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Wasanii wa filamu wamejitokeza kushiriki katika mazishi hayo.

Mzee Jengua alifariki dunia Desemba 15 mwaka huu huko Mkuranga mkoani Pwani baada ya kuugua kwa muda mrefu.