Mamia wamuaga Ngwilizi

0
245

Rais John Magufuli ameongoza mamia ya waombolezaji, kuaga mwili wa aliyekuwa Mwanasiasa mkongwe hapa nchini Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi, aliyefariki dunia Mei 20 mwaka huu katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es salaam.


Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Ngwilizi umeagwa katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es salaam na baadaye kusafirishwa kwenda wilayani Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika hapo kesho.


Akimuelezea Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Ngwilizi, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Phillip Mangula amesema kuwa alikuwa ni kiongozi  mwenye nidhamu  kwenye kazi na alikua ni Mzalendo wa kweli.


Marehemu Brigedia Jenereli Mstaafu Ngwilizi alizaliwa mwaka 1942.