Mamia wajitokeza kumuaga Dkt. Mengi

0
556

Wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro na viunga vyake wameungana na wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhudhuria ibada ya mazishi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, itakayofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – KKKT usharika wa Moshi Mjini mchana wa leo.

Mamia ya watu wanaendelea kutoa heshima zao za mwisho katika Kanisa hilo kabla ya kuanza kwa ibada majira ya saa saba mchana inayotarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Kanisa hilo la KKKT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo.

Baada ya ibada hiyo ambayo inahudhuriwa na wananchi, wafanyabiashara, viongozi wa siasa na serikali mazishi ya Dkt .Mengi yanatarajiwa kufanyika Machame alasiri ya leo.