Mambosasa: Jeshi la polisi lipo imara kuhakikisha utulivu na amani

0
392

Kuelekea uchaguzi mkuu 2020 Watanzania wamehizwa kumtanguliza Mungu ili kuenzi amani iliyohasisiwa na waasisi wa taifa.

Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa wakati kongamano la amani la viongozi wa dini wenye lengo la kuliombea taifa utulivu na amani wakati wa uchaguzi.

Kamanda Mambosasa amesema jeshi la polisi lipo imara kuhakikisha amani ya nchi inalindwa kwa nguvu zote na atakayeipeleka nchi kwenye kwenye shida yeye ndiye atakayeingia kwenye matatizo.

“Watanzania waendelee kumtanguliza Mungu katika uchaguzi mkuu maana yapo maisha mengine baada ya uchaguzi”Amesema

Aidha, amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi limejidhatiti kuilinda na kudumisha amani iliyopo hivyo Watanzania wasiogope kwenda kupiga kura kwa ajili ya kuwapata viongozi wanaowataka.

“Ukitaka kuijua Tanzania nenda nchi za jirani utaona ni kwa namna gani inasifiwa kuwa kisiwa cha Amani,” amesisitiza Mambosasa.