Mambosasa awaonya wanasiasa wanaotaka kuandamana Dar es Salaam

0
398

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewaonya wanasiasa na wafuasi wao wanaotaka kuandamana jijini Dar es Salaam na kusema kuwa jeshi hilo limejipanga kuwadhibiti.


Akizungumza katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere ambapo matokeo ya uchaguzi wa Rais yanatangazwa amesema kuwa baadhi ya wanasiasa wamefanya Dar es Salaam kuwa shamba la bibi. 


“Wengine wamepigiwa Hai, wengine Arusha wamejikusanya Dar es Salaam kama sehemu ambayo ni shamba la bibi wanataka kufanya vurugu”.


Mambo sasa amevionya vikundi hivyo alivyosema vinalenga kuzuia kutangazwa kwa matokeo ya urais na kusema kuwa muda wa kampeni umekwisha na sasa jeshi la polisi limejipanga kulinda raia na mali zao.


Mambosasa amewataka wananchi wa Dar es Salaam kuwapuuza wanasiasa hao, na kama kuna mtu anataka kuingia mtaani amesema aingie yeye na familia yake.