Mambosasa akanusha polisi kugawana nyama

0
217

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa hakuna nyama zilizogawanwa kwa askari polisi wala mtu wa aina yeyote kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.

Katika taarifa yake, Kamanda Mambosasa amesema uchunguzi wa sakata hilo ulioongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es salaam umebaini kuwa nyama hizo ziliteketezwa na nyingine zilifukiwa ardhini.

Wakati wa uchunguzi zile zilizofukiwa zilifukuliwa eneo la tukio ili kuthibitishwa na wapelelezi waliokuwa wanachunguza sakata hilo pamoja na bodi ya nyama na kubaini zilikuwa kilo 110 za nyama na sio kilo 800 ilivyokuwa inasemekana na ndizo zilizojazwa kwenye hati ya kutaifisha (Certificate of Seizure) na watuhumiwa wenyewe.

Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia uwepo wa madai ya polisi kugawana nyama zilizokamatwa kwenye oparesheni ya kukamata watu wanaouza nyama sehemu ambayo hairuhusiwi na mazingira yake ni hatarishi kiafya mkoani Ilala.

Katika oparesheni hiyo oparesheni hiyo iliyofanyika maeneo ya machinjio ya Vingunguti watuhumiwa 14 walikamatwa.