Mamba Aliyesumbua Kijiji Auawa

0
282

Wakazi wa kijiji cha Bukondo wilayani Geita wamemuua mamba aliyeua wakazi Watano wa kijiji hicho kuanzia mwezi Aprili mwaka huu hadi mwezi huu wa Agosti.

Tukio la mwisho ilitokea tarehe Mosi mwezi huu ambapo mtoto mwenye umri wa Miaka Tisa Fabian Kilabu aliyekuwa anasoma darasa la Tatu wilayani Chato aliuawa na mamba huyo.

Afisa Wanyamapori Geita Msese Kaburenzina, amesema wametoa kibali cha kuwaua mamba hao kutokana na viashiria vya watu kuuawa.