Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa changamoto mbalimbali zitokanazo na muungano si jambo baya.
Akizungumza katika kikao cha kusaini hati tano za makubaliano kwa ajili ya kuondoa hoja za muungano zilizopatiwa ufumbuzi, Mama Samia amesema, “haimaanishi kuwa Muungano wetu una matizo, bali ni kurekebishwa kwa kasoro au changamoto hizo.
“Nasema hivi kwasababu hata kwenye nyumba zetu hakukosekani migongano, lakini tunapozungumza na kurekebisha kasoro zetu, migongano inaondoka na nyumba zinaendelea.”
Aidha, Makamu wa Rais ameagiza wizara zenye hoja ambazo hazijapatiwa ufumbuzi, kuzitafutia ufumbuzi hoja hizo