Malima: Sheria ya Bima iangaliwe

0
779

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema, kuna haja ya kuiangalia upya sheria ya Bima hasa kwenye ulipaji wa fidia pindi ajali zinapotokea.

Malima amesema kumekuwa na ucheleweshaji wa malipo ya fidia kwa kampuni za Bima kwa wateja wanaokatia Bima vifaa vyao hasa magari na vyombo vingine vya moto.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ametoa rai hiyo wakati akihitimisha wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa mkoani Mwanza.

Amelitaka Jeshi la Polisi nchini kushirikiana na wadau wa Bima kuliangalia jambo hilo.

Malima amesema watu wengi wanakata tamaa kukata Bima za mali zao kutokana na uchelewashwaji wa fidia kutoka kampuni za Bima pindi wanapopata ajali zinazopaswa kufidiwa.